ElimuTaifa
TAARIFA ZA ELIMU

Matangazo na taarifa za elimu

Habari, matokeo, selection na admission — pata taarifa muhimu katika sehemu moja.

6 taarifa

Tangazo

✨ MWANGA MPYA KUPITIA MNUBY FOUNDATION! ✨

Unahitaji msaada wa masomo au ushauri wa kitaaluma? Mnuby Foundation inakaribisha maombi ya wanafunzi wanaojiandaa na masomo ya elimu ya juu na sekondari.

Soma taarifa kamiliClose
The Founder, Mnuby Foundation
The Founder, Mnuby Foundation
✨ MWANGA MPYA KUPITIA MNUBY FOUNDATION! ✨ Unatafuta msaada wa masomo, mwongozo, au ushauri wa kitaaluma ili kufikia ndoto zako? Usihangaike tena! Mnuby Foundation inakaribisha rasmi maombi na kuwakaribisha wanafunzi wote wanaojiandaa na masomo ya elimu ya juu na sekondari. Tunakusaidia kupata mwelekeo sahihi wa kimasomo na kukupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi. 🎯 Nafasi ni kwa ajili yako. Kua kimasomo na Mnuby Foundation leo! 👉 Soma taarifa kamili na kupata ufafanuzi zaidi kupitia ElimuTaifa.
Tangazo

RUSSIAN STATE SCHOLARSHIP PROGRAMME 2027/2028

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa taarifa rasmi kuhusu udhamini wa masomo nchini Urusi kwa mwaka wa masomo 2027/2028.

SourceWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Soma taarifa kamiliClose
INFORMATION
INFORMATION
Walengwa: Watanzania wenye sifa wanaokaribishwa kuomba nafasi za masomo ya Shahada ya Kwanza (Undergraduate) na Shahada za Uzamili (Postgraduate) katika vyuo vikuu nchini Urusi kupitia nyanja mbalimbali. Ufadhili (Scholarship Coverage): Huu ni ufadhili wa sehemu (partial scholarship) unaogharimia ada ya masomo pekee. Wanafunzi watakaofanikiwa watapaswa kujigharamia malazi, posho za kila mwezi, usafiri, bima ya afya, vifaa vya kusomea, na gharama za visa. Kumbuka Muhimu: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitoi mikopo wala ruzuku ya kuongezea kwenye udhamini huu. Dirisha la Maombi: Kufunguliwa: 15 Novemba 2026 Kufungwa: 15 Januari 2027 Tovuti ya Maombi: Unaweza kutembelea Tovuti Rasmi ya Scholarship ya Urusi kwa maelezo zaidi na taratibu za kutuma maombi. 🌐https://education-in-russia.com
Uzinduzi wa Mwongozo wa Elimu ya Fedha kwenye Elimu ya Juu na VETAFungua video kwenye YouTube
Habari mpya

Uzinduzi wa Mwongozo wa Elimu ya Fedha kwenye Elimu ya Juu na VETA

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imezindua mwongozo wa kuchopeka elimu ya fedha katika mitaala ya elimu ya juu na vyuo vya ufundi (VETA) ili kuwaandaa vijana kuwa na nidhamu ya kifedha na stadi za kibiashara.

SourceTBConline
Soma maelezo ya videoClose
Uzinduzi wa Mwongozo wa Elimu ya Fedha kwenye Elimu ya Juu na VETA Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imezindua mwongozo wa kuchopeka elimu ya fedha katika mitaala ya elimu ya juu na vyuo vya ufundi (VETA) ili kuwaandaa vijana kuwa na nidhamu ya kifedha na stadi za kibiashara. Mambo Muhimu: Lengo: Kuwajengea vijana uwezo wa kusimamia rasilimali, kuweka akiba, na kujiajiri baada ya kuhitimu. Utekelezaji: BOT inashirikiana na wizara, TCU, na bodi ya mikopo kupima matokeo ya mabadiliko ya kifedha kwa wanafunzi. Dira ya Taifa: Elimu hii ni kichocheo kikuu cha Dira ya 2050 kuandaa wawekezaji na walipa kodi bora.
Habari mpya

Mabadiliko ya Kumaliza Elimu ya Msingi (Mwaka 2027)

Kulingana na taarifa rasmi kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023 pamoja na mitaala iliyoboreshwa), yafuatayo ni mabadiliko kwa wanafunzi watakaomaliza elimu ya msingi mwaka 2027

SourceNECTA PAGES
Soma taarifa kamiliClose
INFORMATION
INFORMATION
Kulingana na taarifa rasmi kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023 pamoja na mitaala iliyoboreshwa), yafuatayo ni mabadiliko kwa wanafunzi watakaomaliza elimu ya msingi mwaka 2027: Wanafunzi wa Darasa la Tano (Mwaka Huu): Kupitia mitaala mipya, wanafunzi waliopo Darasa la Tano mwaka huu watamaliza elimu yao ya msingi mwaka 2027 wakiwa bado wako Darasa la Sita. Wanafunzi wa Darasa la Sita (Mwaka Huu): Wanafunzi waliopo Darasa la Sita mwaka huu watakuwa kundi la mwisho kusoma na kumaliza kupitia mfumo wa zamani hadi Darasa la Saba mwaka 2027. Endelea kutembelea ElimuTaifa kupata taarifa za kuaminika za elimu, matokeo, na selection nchini Tanzania!
Wanafunzi wa Darasa la Pili, la Nne na Kidato cha Pili kufanya Upimaji wa Kitaifa Oktoba 2026Fungua video kwenye YouTube
Tangazo

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi ratiba ya upimaji wa kitaifa kwa mwaka 2026 kama ifuatavyo:

SourceYOUTUBE NECTA ONLINE
Soma maelezo ya videoClose
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi ratiba ya upimaji wa kitaifa kwa mwaka 2026 kama ifuatavyo: Darasa la Pili (Standard 2 National Assessment): Utafanyika tarehe 7 na 8 Oktoba, 2026. Darasa la Nne: Utafanyika tarehe 5 na 6 Oktoba, 2026. Kidato cha Pili (Form 2): Utafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 23 Oktoba, 2026. Mambo muhimu ya kuzingatia: Usajili: Mamilioni ya wanafunzi wamesajiliwa kote nchini, huku kukiwa na maandalizi maalumu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (ikiwemo nukta nundu kwa wasioona na muda wa ziada). Uadilifu: Baraza limeweka mikakati thabiti kuzuia udanganyifu. Uongozi wa shule umeonywa kutuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani, na yeyote atakayebainika kuhujumu mitihani atachukuliwa hatua kali za kisheria. Wito kwa Umma: Wananchi wameombwa kushirikiana na baraza kutoa taarifa za vitendo vya udanganyifu kupitia namba ya simu 0759 3600 au barua pepe esnctta@necta.go.tz.
Habari mpya

Updates za Mitihani ya Taifa (Necta)

Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA): Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Darasa la Nne 2026 katika Upimaji wa Kitaifa uliofanyika kuanzia tarehe 05 hadi 06 Oktoba, 2026.

SourceNECTA PAGES
Soma taarifa kamiliClose
Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA)
Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA)
Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA): Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Darasa la Nne 2026 katika Upimaji wa Kitaifa uliofanyika kuanzia tarehe 05 hadi 06 Oktoba, 2026. Mitihani ya Darasa la Pili: Taarifa maalum zilizotolewa zinaonyesha kuwa maandalizi na ratiba za Mitihani ya Darasa la Pili ziko njiani kuanza hivi karibuni. Ujumbe Mkuu: Ni kipindi muhimu cha kuendelea kufuatilia matokeo na taarifa nyingine za elimu kupitia vyanzo rasmi vya Baraza la Mitihani na tovuti ya Elimu Taifa.
WhatsApp Channel